FAO in Tanzania

FAO yahimiza matumizi ya teknohama katika kudhibiti kiwavi jeshi vamizi nchini

Wakulima wakipewa mafunzo ya namna ya kutumia programu hii ya simu
27/11/2018

Tanzania imekua mhanga wa mashambulizi ya kiwavi jeshi vamizi nchini kwa muda wa miaka miwili sasa. Asili ya mudu huyu ni bara la Amerika kusini. Mpaka sasa kiwavi jesho vamizi kimeshashambulia zaidi ya nchi 28 duniani zenye mazingira rafiki kwa ukuaji wake. Hasara za kiuchumi zinazitokana na mdudu huyu huenda zikafikia  thamani ya kiasi cha dola billioni 4.8 kwa mwaka kwa bara la Afrika kwenye mahindi pekee. Mhanga mkubwa zaidi wa uharibifu huu ni mkulima mdogo. Kutokana na uwezo mkubwa wa kipepeo kinachitaga mayai ya kiwavi jeshi vamizi kuvuka mipaka, zinahitajika jitihada za kitaifa  na za kimataifa kumdhibiti.

Asili yake

Tueleze kidogo kuhusu asili yake na kisha athari zake yake kwa undani kwa kutoa mifano michache ya hata hapa hapa nchini ndio tuingie kwenye njia za kuwadhibiti.

Hatua ya kwanza ya kufanya maamuzi ya udhibiti ni kubaini uwepo wake na kutumia mbinu za udhibiti husishi kama vile madawa ya kemikali, kusaga mayai na viwavi, matumizi ya mitego yenye chambo na kufukua mabuu ya mdudu kuzuia kutoka kwa kipepeo. Juhudi mbali mbali zinafanyika zikijumuisha Serikali na Wadau mbali mbali katika kudhibiti tatizo hili. Kwa mfano, Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) limekua likiendesha mafunzo juu ya udhibiti wa mdudu huyu barani Afrika na kutoa mitego, chambo na dawa kwa wakulima nchini.

Ili kufahamu endapo jitihada hizi zinazaa matunda ulionekana umuhimu wa mkulima kutumia mbinu hizi za udhibiti na kutuma taarifa za mwenendo wa kiwango cha mashambulizi shambani kwake mara kwa mara. Ili kuwezesha hili, FAO imetoa programu ya simu iitwayo FAMEWS itakayomuwezesha mkulima kutuma taarifa hizi mara kwa mara kila akaguapo shamba lake. FAO imeshatoa simu janja 84 kwa wakulima mbali mbali nchini kuwasaidia kwenye matumizi ya program hii ya kimapinduzii

“Kwa kutumia mfumo huu, mkulima anaweza taarifa kuhusu shamba lake, hali ya hewa wakati wa msimu, msaada aliopokea kutoka kwa wadau wa kilimo na serikali pamoja na kiwango cha uharibifu shambani kwake mara kwa mara,” anasema Bw. Baitani Mushobozi, Afisa Afya ya Mimea wa FAO Tanzania

Umuhimu wa taarifa

Anasema kuwa taarifa hizi zitasaidia serikali utuma na wadau wa maendeleo kutambua maeneo yanayoshambuliwa kwa wingi, maeneo yaliyopokea msaada na yapi bado, kugundua mashambulizi mapya mapema, mwenendo wa mashambulizi kupanda ama kushuka, mbinu zinazofanya kazi na kisha kuchukua hatua stahiki mapema ili kumpunguzia mkulima hasara.

Kwa mujibu wa Afisa huyu wa FAO Tanzania, kanzidata ya taarifa zinazokusanywa kwa FAMEWS itaweza kusaidia wadau kujipanga kumsaidia mkulima katika namna itakayoleta tija. Hivyo FAO inakaribisha wadau wote kumfundisha mkulima matumizi ya mfumo huu.  

“Kwa taarifa hizi, rasilimali zitatumika zaidi sehemu zinazohitajika, itapunguza mlundikano wa misaada kutoka kwa wadau kwenye eneo moja na kusaidia utekelezaji wa mipango itakayoweza kufikia wakulima wengi Zaidi,” anaongeza.  

Programu ya FAMEWS kwa sasa inapatikana kwenye simujanja za aina zote. Mkulima yoyote aliyeshambuliwa na mdudu huyu anahimizwa atumie fursa hii kutoa taarifa mapema juu ya mwenendo shambani kwake. Shirika la FAO limetoa kompyuta ya kisasa kwa Wizara ya Kilimo ili waweze kupokea taarifa hizi na kuzifanyia kazi kwa wakati na usahihi kwa faida ya mkulima. Kwa matumizi haya ya teknohama katika kupeana taarifa, vita dhidi ya mdudu huyu itakua na nafasi kubwa ya kufanikiwa.